Naibu
Waziri wa Fedha Mh;Mwigulu Nchemba akiwa ameongozana na Naibu Kamishina
Idara ya Forodha na Ushuru wa Bidhaa Tanzania,Ndugu Patric
Kisaka(kulia) na Mkurugenzi wa huduma za Ulipaji Kodi na Elimu
Ndugu,Richard Kayombo pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kyela Bi.Magreth
Kalenga(hayupo pichani) wakiondoka kwenye Ofisi za TRA Kuelekea kwenye
eneo la Mpakani Mwa-Tanzania na Mawali wilayani Kyela hii leo.
Kibao Kianachoonesha "KARIBU TANZANIA" kilichopo pembezoni mwa Mto Songwe unaotumiaka kama mpaka wa Tanzania na Malawi.
Huu
ndio Mto Songwe ambao ni Mpaka wa Tanzania na Malawi Wilayani Kyela.Huu
mto umeleelekea hadi Ziwa Nyasa na ndio Mpaka wa Tanzania na
Malawi,Lakini sehemu kubwa ya Mto huu kunavipenyo visivyo rasmi
vinavyotumika na Wananchi Kuvusha Biashara za Magendo na Kukwepa kulipa
kodi kwa kupita kwenye Kivuko rasmi cha Kasumulu hapa Kyela.
Msafara
wa Naibu Waziri wa Fedha umefika kwenye hiki Kipenyo cha Mto
Songwe(Kinajulikana kama Timotheo) kinachotumika na Wananchi wasio
wazalendo Kuvusha bidhaa mbalimbali kutoka Tanzania -Malawi au Malawi
kuja Tanzania.Ng'ambo ya Mto unaonekana ni mzigo mkubwa wa sukari
unaotarajiwa Kuvushwa kuja Tanzania kwa njia za Magendo na kubwa zaidi
Kukwepa Ulipaji Kodi.
Naibu
Waziri wa Fedha akiangalia Moja ya Mtumbi unaotumiaka kuvushia Biashara
za Magendo kwenye hiki kivuko haramu cha Timotheo kwenye Mto Songwe.
Naibu
Waziri na Msafara wake wakiwa kwenye Kivuko Kingine kisicho rasmi
kinachotumika Kuvushia bidhaa za magendo kutoka Nchi hizi mbili za
Tanzania na Malawi.Ng'ambo kwenye Nyumba zinazoonekana ni Nyumba za
Wananchi wa Malawi.Na kwa mbali kunaonekana roli likiwa limepakia Mzigo
unaodaiwa kuwa ni Mpunga uliovushwa kwa Magendo kutoka Tanzania kwenda
Malawi.
Naibu
Waziri wa Fedha Mh:Mwigulu Nchemba akifanya mahojiano na Vijana
waliokutwa wakivusha sukari kutoka Malawi kuja Tanzania.Vijana hao
wanadai wanalazimika kutumia njia hizi haramu kuvusha Sukari kutokana na
kuwa na mitaji midogo ya biashara zao,Hivyo kupita kwenye Kivuko Rasmi
cha Kasumulu wanakatwa Kodi Kubwa ambayo inawafanya wakose faida kwenye
Biashara yao.
Naibu
Waziri wa Fedha akizungumza na Watumishi/Watendaji wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania na Watumishi wa Idara mbalimbali zinazohusika na Mpaka wa
Tanzania na Malawi.
Na.Habari Kwanza Blog,
Naibu
Waziri wa Fedha Mh:Mwigulu Lameck Nchemba hii leo(Tar.04/02/2014)
ameendelea na Ziara yake ya Kikazi Mkoani Mbeya ya Kutembelea Vituo vya
Ukusanyaji wa Mapato na Kuangalia changamoto za Ukusanyaji wa mapato
kwenye maeneo ya Mipaka ya Nchi.
Hii
leo amefika Wilaya ya Kyela na kukutana na Mkuu wa Wilaya Mh:Magreth
Kalenga aliyeongoza kutembelea maeneo ya Mpaka wa Tanzania na Mawali
kutathimini namna Ukusanyaji wa Mapato unavyokuwa na changamoto nyingi
kutokana na Watanzania wengi kukwepa Kulipa kodi kwenye Vivuko rasmi vya
Mipaka.
Wilaya ya Kyela imetajwa kuwa na Vipenyo visivyo rasmi 32 vinavyotumika kupitisha bidhaa za magendo(sukari, Viroba,Mpunga n.k) ,Katika
hali ya kuonesha kuwa biashara ya Magendo imeshamili mpakani hapo,Naibu
Waziri wa Fedha ameshuhudia vijana wakivusha Sukari kutoka Malawi kuja
Tanzania kwenye kipenyo kisicho rasmi kinachojulikana kwa jina la
Timotheo.Katika mahojiano ya Mh;Mwigulu na Vijana hao,Watanznaia hao
wanasema walazimika kutumia njia hizo za panya kuvusha bidhaa hizo
kwasababu ya Ushuru kuwa Mkubwa na Mtaji wao ni mdogo,pia Ugumu wa
Maisha ndio unawafanya wakimbilie kutafuta faida ya haraka ilikusaidia
familia zao.
Naibu Waziri amesema Kupitia Wizara yake(Serikali) imejipanga kufanikisha haya.
1.Kuhakikisha
upatikanaji wa bidhaa(Sukari n.k) nchini unaongezeka ilikutoa nafasi
ya wafanyabiashara kuchana na biashara za magendo za kutumia bidhaa za
Malawi kwa njia ya kukwepa kodi.
2.Kuongeza
Watumishi wa Kwenye Mipaka wanaohusika na Usalama,Ukusanyaji wa Mapato
n.k ilikuhakikisha huduma zinatolewa kwa wakati bila usumbufu wowote.
3.Pia
Ujenzi wa kituo kituo cha Pamoja(One-Stop Border Post) cha Ukaguzi kati
ya Nchi ya Tanzania na Malawi ilikuondoa Urasimu na Ucheleweshwaji wa
kupitisha bidhaa kwenye vivuko vya Mipakani.Mazungumzo yameshaanza na
Utekelezaji unategemea kuanza mapema.
3.Kuongeza
Upatikanaji wa Elimu kwa Wafanyabiashara kuhusu athari za kukwepa
kodi,faida za kutumia Vivuko rasmi kwenye upitishaji wa bidhaa zao.
Hongera kk mheshimiwa kwa kazi nzuri, najua una kazi ngumu. MUNGU atakusaidia , tupo pamoja kaza buti
ReplyDeleteKazi nzuri Mh.Nakutakia kila la heri.
ReplyDelete