Naibu
waziri wa Fedha Mh;Mwigulu Nchemba akisisitiza jambo kwa
Wafanyabiashara wa Mji wa Tunduma hii leo alipokutana nao kwenye Mkutano
wa ndani kwenye Ukumbi wa High Class One akizungumza nao kuhusu
Maendeleo ya Biashara,Ulipaji wa kodi,Changamoto za Mpakani kwenye
Ulipaji kodi,matumizi ya Mashine za EFD kwenye makato ya TRA.
Sehemu
ya Mamia ya Wafanyabiashara waliohudhuria Mkutano wa Naibu Waziri wa
Fedha Mh;Mwigulu Nchemba wa Kujadiliana na kuelezana namna ya Kuimarisha
Ukusanyaji wa mapato nchini.
Naibu
Waziri wa Fedha Mh:Mwigulu Lameck Nchemba hii leo ameendelea na Ziara
yake ya kikazi ya Kukutana na Wafanyabiashara ndnai ya Mkoa wa Mbeya
baada ya Kufanya hivyo kwenye Mkoa wa Njombe na Ruvuma wiki iliyopita.
Hii
leo Mh:Mwigulu amezungumza na mamia ya wafanyabiashara wa Mji wa
Tunduma kuhusu nafasi yao ya Kukuza Ukusanyaji wa mapato kwa kaucha
kukwepa kulipa kodi,Kuacha kupitisha bidhaa kimagendo kwenye mpaka wa
Nchi ya Tanzania na Zambia.Wafanyabiashara Wakitanzania wasio wazalendo
wa Kulipa kodi wamekuwa wakitumia mwanya wa Mpaka kuvuka kufanya
biashara Zambia na makazi yao yapo Tanzania kitu kinachopelekea
ukusanyaji wa Mapato kuwa Mgumu kwa TRA na taasisi husika. Serikali
imeamua kufanya maridhiano na Serikali ya Zambia kuhakikisha kunakuwepo
na Mpaka uliotenganishwa kwa Mita 50 kila upande wa Nchi hizi mbili
ilikudhibiti ukwepaji wa kulipa kodi na biashara ya Magendo.
Naibu
waziri pia alitumia nafasi kuwaelimisha Wafanyabiashara umuhimu wa
kutumia mashine za EFD kwenye kurahizisha ukusanyaji wa mapato na kukuza
biashara zao.Mbali na hayo wafanyabiashara walipata nafasi ya kutoa mawazo,maoni yao kwa Naibu waziri wa Fedha namna ya Kuimarisha Ukusanyaji wa mapato,Uelewa wao kuhusu Mashine za EFD na Ushirikiano watakao onesha kwenye Kudhibiti ukusanyaji mapato mpakani Mwatanzania na Zambia.
Picha na Habari Kwanza Blog
No comments:
Post a Comment