Naibu
Waziri wa Fedha(sera) Mh:Mwigulu Lameck Nchemba akiwa katika picha ya
pamoja na Wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoani Mbeya
mapema hii leo.
Naibu
Waziri wa Fedha Mh:Mwigulu Nchemba akiwasili Ofisi za Mamlaka ya Mapato
TRA Mkoani Mbeya hii leo wakati wa Ziara yake ya Kikazi ya kutembelea
Ofisi zote za TRA,Ofisi za Hazina ndogo na Kuzungumza na Wafanyabiashara
katika Mikoa ya Njombe,Ruvuma na Sasa Mbeya.
Naibu
Waziri wa Fedha Mh:Mwigulu Nchemba akizungumza na Watendaji/watumishi
wa TRA,Hazina ndogo,Takwimu na Uhakiki Mali Mkoani Mbeya mapema hii leo
asubuhi.
Na,Habari Kwanza Blog.
Naibu
Waziri wa Fedha (Sera) Mh;Mwigulu Nchemba hii leo asubuhi
(Tar.05/02/2014) amekutana na Watendaji/Watumishi wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania(TRA),Hazina Ndogo na Wahakiki Mali za Serikali Mkoani Mbeya
Kwaajili ya Kufahamiana nao,pia Kuzungumza nao kuhusu Uboreshaji wa
Ukusanyaji wa Mapato Nchini,Msimamo wa Serikali kuhusu Matumizi ya
Mashine za EFD kwenye Ulipaji kodi,Pia Uadilifu na Ushirikiano katika
Utumishi wa Umma hususani kwenye Wizara ya Fedha.
Akizungumza
na Watendaji hao,Naibu Waziri amesema,Serikali imejipanga na itaendelea
kusimamia zoezi la kuhakikisha Wafanyabiashara wanatumia mashine za EFD
ilikukusanya kodi halisi ya bidhaa/huduma wanazotoa kwa
Wananchi.Utumiaji wa mashine za EFD kwa wafanyabiashara unaboresha
kipato halisi cha bidhaa wanazoziuza,pia mashine zinasaidia kudhibiti
mianya ya Ukwepaji wa kulipa kodi Nchini.
Kwa
Mkoa wa Mbeya wenye Wafanyabiashara walipa kodi waliojiandikisha 32647,
kuna zaidi ya Wafanyabiashara 297 walionunua mashine za EFD na zaidi ya
300 wameshaanza kulipa kwa awamu iliwaweze kupatiwa mashine hizo,Idadi
hii ya wanunuzi wa Mashine za EFD imeongezeka kwa kasi mara baada ya
Mgomo wa Wafanyabiashara uliofanyika 1/10/2013 kupinga matumizi ya
Mashine hizo.TRA kupitia mawakala wake wamekuwa wakitoa Elimu ya
Matumizi ya mashine hizo kwa wafanyabiashara na hatimaye uelewa umekuwa
mkubwa na sasa wengi wamejitokeza kununua mashine hizo.
Pia
Mh:Mwigulu Nchemba amesisitiza Ushirikiano na Umoja kwenye Utumishi wa
Ofisi za Umma hususani hizi za Ukusanyaji wa kodi Nchini.Haikubaliki kwa
Mtendaji/mtumishi wa TRA na idara husika za mapato kufanya ubadhirifu
wa kodi za Watanzania wakati serikali inatumia nguvu kubwa kuhakikisha
kodi Inakusanywa kwenye vyanzo vyote.Ni wajibu kwa kila Mtumishi kufuata
sheria za Nchi za Utumishi ilikuondokana na adha atakayoipata pindi
Ofisi yake ikibaini kuna watendaji wanaofanya ubadhirifu wa kodi za
Watanzania.
No comments:
Post a Comment