Naibu
Waziri wa Fedha Mh:Mwigulu Nchemba akizungumza na Wafanyabiashara wa
Mbeya Mjini hii leo kwenye Ukumbi wa Mtenda Hotel Jijini Mbeya.Sehemu ya Wafanyabiashara wa Mbeya Mjini wakiwa kwenye Mkutano wa ndani wa Naibu Waziri wa Fedha Mh.Mwigulu Nchemba hii leo.
Naibu
Waziri wa Fedha Mh:Mwigulu Nchemba hii leo amehitimisha ziara yake ya
kikazi iliyojumisha Mikoa Mitatu(Njombe,Ruvuma na Mbeya),Ziara yake
imehitimishwa kwa Kuzungumza na Wafanyabiashara wa Mbeya Mjini,Pia
amekutana na Watendaji/watumishi wa Mamlaka ya mapato
Tanzania(TRA),Hazina ndogo Mkoani Mbeya na Ofisi ndogo ya Takwimu.
Akizungumza
na Wafanyabiashara wa Mbeya Mjini Naibu Waziri amesema,Katika ziara
yake amesisitiza kuwa Ofisi yake inatambua Mchango wa Wafanyabiashara
katika Uchumi wa Nchi hii hususani ulipaji wa kodi,Hivyo katika utungaji
wa Sera mbambali za ulipaji kodi na Kuinua Uchumi wa Nchi, Ofisi yake
itashirikiana na Wafanyabiashara nchi nzima kwasababu ndio wadau husika
kwenye ulipaji kodi katika Taifa hili.
Pia
Mh:Mwigulu ameendelea kuwaomba Wafanyabiashara kuendelea kuunga mkono
matumizi ya Mashine za EFD's kwenye ukusanyaji wa kodi halisi za
bidhaa/huduma husika inayotolewa.Ni muhimu kwa Watanzania kutambua
mabadiriko ya mifumo ya ukusanyaji kodi nchini kwa manufaa yao na Taifa
lao,Kutumia mashine za EFD's kunasaidia kudhibiti upotevu wa mapato
kupitia kodi,Kunasaidia wafanyabiashara kupata makusanyo stahiki
kulingana na huduma/bidhaa anazouza.
Akiwa
ameambatana na Wataalamu kutoka Wizarani na Makao Makuu ya
TRA,Wafanyabiashara wa Mbeya wameelimishwa kuwa Mfanyabiashara yeyote
mwenye mauzo kuanzia Milioni 14 kwa Mwaka ndiye anapatwa kutumia mashine
hizo,Pia wafanyabaishara wote waliosajiliwa kulipa kodi,Pia matumizi ya
Mashine za EFD's zinasaidia kutunza kumbukumbu za biashara
husika,Zinapunguza wizi na Ujanja wa wauzaji wasio wenye mali.
Vilevile,Wafanyabiashara
wa Mbeya wameomba serikali kuondoa ufutiliaji wa kulipa kodi kwa
wachuuzi wadogowadogo,Serikali ifanyie kazi Ukusanyaji wa Kodi kwenye
Viwanda,Mipakani,Viwanja vya Ndege na kwenye Soko la kimataifa.Pia
sheria ya Kodi ni kandamizi kwa Wafanyabiashara wa dogowadogo na faini
zake ni kubwa mno kitu kinachoshawishi Rushwa kati ya Wafanyabiashara na
Watendaji wa TRA.
Chanzo:Habari Kwanza Blog
No comments:
Post a Comment