Naibu
Waziri wa Fedha akizungumza na Wafanyabiashara hii leo Wilayani Kyela
kuhusu Matumizi ya Mashine za EFD na Umuhimu wa Kulipa kodi kwenye
Biashara zao.
Sehemu
ya Wafanyabiashara wa Wilaya ya Kyela waliofika kwenye Mkutano wa
Mh;Mwigulu Nchemba Naibu Waziri wa Fedha(Sera) hii leo.
Naibu
Waziri wa Fedha Mh:Mwigulu Nchemba hii leo amekutana na Wafanyabiashara
wa Wilaya ya Kyela katika mwendelezo wa ziara yake ya Kikazi ya
kukutana na Watendaji wa Mamlaka ya Mapato(TRA),Wafanyabiashara na
Watendaji wa Ukusanyaji wa Ushuru wa Forodha(mipakani).
Akizungumza
na Wafanyabiashara wa Kyela,Mh:Mwigulu Nchemba amewatoa hofu
wafanyabiashara kuhusu Matumizi ya Mashine za EFD kwenye Biashara
zao,amesisitiza kuwa Kukosena kwa Elimu ya Kutosha kuhusu Mashine hizo
kumepelekea Wafanyabiashara wengi kulalamika hata kabla ya Kununua
mashine zenyewe.Mashine za EFD zimeidhinishwa na Mamlaka ya Mapato
kutumika kwenye ununuzi wa bidhaa kwa wateja ilikudhibiti ulipaji wa
kodi za bidhaa na huduma mbalimbali za kibiashara.
Mh:Mwigulu
amewaeleza Wafanyabiashara wa kyela kuwa Mashine za EFD ni bora sana
hasa kwa kukuza faida kwa Wafanyabiashara kupitia ulipaji Kodi usiokuwa
na vikwazo.Amewaomba wananchi kununua mashine hizo kwa haraka sana na
TRA imejipanga kutoa huduma kwa ukaribu zaidi kwa yeyote atakayekuwa na
tatizo na mashine hizo za kukusanyia mapato ya kodi.
Pia
Naibu Waziri wa Fedha ametaka Wakazi wa Kyela kaucha kutumia njia za
panya kupitisha bidhaa zao,Kitendo cha kutumia vipenyo vya mto Songwe
kukwepa kulipa Kodi ni kitendo cha kuhujumu Uchumi wa Nchi,Pia ni Kosa
kisheria kuingiza bidhaa ya nje ya nchi bila idhini ya Serikali ya
Tanzania kupitia Idara zake za Ushuru wa Forodha.Hivyo ni muhimu
kuachana na mchezo huo wa kuhujumu Uchumi,Serikali ya Tanzania na Malawi
zimejipanga kuhakikisha ushuru wa Forodha na kodi mpakani utakuwa
unakusanywa kwa Kituo Kimoja cha pamoja(One-Stop Border Post)
ilikurahizisha upitishaji wa Mizigo mpakani Mwanchi hizi mbili.
Mbali
na hapo,Serikali inachukua hatua za kuangalia namna ya kuhakikisha
bidhaa zinazovushwa kwa magendo(Sukari n.k) zisizo na athari kwa
Watanzania zitatafutiwa namna ya kupatikana kwa Wingi ilikuondokana na
uingizaji wa Bidhaa kwa njia za Magendo.
Vilevile
Soko la Mchele linatafutiwa dawa ya Kudumu kwa Wafanyabiashara
wote,Serikali imesikia kilio cha wauzaji wa mchele hasa kitendo cha
kuingiza Mchele wa nje ya Nchi na kusababisha soko la Mchele wa ndani
kuwa gumu kwa Watanzania wenzetu.
Awali
Mbunge wa Kyela Mh:Waziri wa Uchukuzi Harrison Mwakyembe akizungumza na
Watendaji wa Halmashauri ya Kyela,TRA na Watumishi wengine alisema
"Nimeshangwaza sana na Wafanyabiashara kukataa kutumia mashine za EFD
wakati ndio mkombozi wa baisharazao na Ulipaji Kodi kwa Nchi
yao.Nimeshangazwa zaidi hata wauza maandazi,Machinga wa
barabarani,Wauzaji wa Viatu wanaotembeza nao wanalalamika mashine za EFD
wakati wao haziwahusu kabisa kabisa,Naomba TRA watoe elimu ya
Kutosha,Wafanyabishara wengi wanarubiniwa,kudanganywa na Watu wachache
kuhusu Mashine za EFD za kukusanyia mapato kwa sababu Wachache hao ni
wale waliokubuhu kukwepa Kodi hapa Nchini.Hivyo Watanzania tumieni
mashine za EFD kukuza Uchumi wa Nchi yetu kupitia mapato ya Kodi.
Chanzo:Habari Kwanza Blog
No comments:
Post a Comment