Monday, 3 February 2014

PICHA:NAIBU WAZIRI WA FEDHA MH:MWIGULU NCHEMBA,AANZA KUWASHUGULIKIA WAKWEPAJI KODI MPAKANI(TANZANIA NA ZAMBIA)

Naibu Waziri wa Fedha Mh;Mwigulu Nchemba akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Momba Mh'Abiud Saidea kuhusu Changamoto za Ukusanyaji wa Mapato Mpakani Mwa-Tanzania na Zambia Tundumba,Mkoani Mbeya.Naibu Waziri wa Fedha Mh;Mwigulu Nchemba akipewa maelekezo kuhusu Upimwaji wa Viwanja uliofanyika na Halmashauri ya Mbozi Kwenye Mpaka wa Tanzania na Zambia .
Naibu Waziri akiangalia Jiwe la Msingi la Mpaka lililopo Mpakani Mwa Tanzanzania na Zambia(Getini).
 Moja ya Alama ya Mpaka kati ya Zambia na Tanzania lillilopo katikati ya Makazi ya Watu(Watanzania na Wazambia).

 Na.
Naibu Waziri wa Fedha Mh:Mwigulu Nchemba hii leo amefanya Ziara ya Kikazi Wilaya ya Momba(mpya) Mkoani Mbeya Kuzungumza na Watendaji wa TRA na Wafanyabiashara wa Mji wa Tunduma mpakani Mwatanzania na Zambia.Katika hatua ya awali Mh:Naibu Waziri ametembelea maeneo ya Mpaka wa Zambia na Tanzania kuangalia namna zoezi la Ukusanyaji wa mapato kwa wafanyabiashara linavyokuwa gumu kutokana na eneo la Mpakani kutumika na Wananchi wa pande zote mbili kibiashara na makazi jambao linaliporekea.
1.Kushamiri kwa biashara za Magendo hivyo kuliingizia hasara Taifa.
2.Ukwepaji Mkubwa wa Kodi kwa Wafanyabiashara kutokana na wengi wao kufanya biashara Tanzania na Wanaishi ng'ambo(Zambia),Wengine ni watanzania wanafanyabiashara zao ng'ambo ya mpaka(zambia) na Kuishi Tanzania.
Tatizo kubwa linalopelekea Ugumu huo wa ukusanyaji wa mapato ni kukosekana kwa (freezone) ya kutenganisha Makazi ya Watanzania na Wazambia.Hivi karibuni Serikali ya Tanzania na Zambia imeingia kwenye makubaliano ya Kutenganisha mita 50 pande zote mbili ilikuweka eneo la wazi la mpaka kwaajili ya kudhibiti mapato na biashara za magendo.
Picha,hapo juu ni(Spot-line) za awali zinazoonesha mpaka wa Tanzania na Zambia zilizowekwa kwa makubaliano ya serikali zote mbili.Hivi sasa serikali inajiandaa kulipa fidia kwa Wananchi wote watakao vunjiwa makazi yao yaliyondnai ya mita 50 pande zote mbili za Nchi hizi rafiki.
Naibu Waziri Fedha Mh:Mwigulu Nchemba amesema kwa upande wa serikali itahakikisha inahimiza vikao vya maridhiano vinavyoendelea vya makatibu wakuu wa Nchi zote mbili(Tanzania na Zambia) kuhusu kuweka eneo la wazi la Mpaka ilikuondoa changamoto zinaoendelea sasa za Ukusanyaji wa mapato,Ukwepaji kodi na biashara za magendo.
Picha zote na Habari Kwanza Blog

No comments:

Post a Comment